Swali: Je, ni sahihi mtu kuitwa jina la ´Abdus-Sattaar na ´Abdus-Sittiyr?

Jibu: Jina ´Abdus-Sittiyr halina tatizo. Ama jina´Abdus-Sattaar hadi sasa sijaona ushahidi wowote wa jina hilo, ingawa linatumiwa na watu. Allaah ndiye as-Sittiyr (Mwenye kusitiri)[1]. Lakini sijapata Hadiyth iliyotaja hivo mpaka hivi sasa.

[1] Ya´laa amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu akikoga sehemu ya wazi pasi na shuka ya chini. Hivyo akapanda juu ya mimbari, akamuhimidi Allaah na kumsifu. Kisha akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) ni Mwenye haya na Mwenye kusitiri (Sittiyr) na anapenda staha na kusitiri. Hivyo basi, atakapooga mmoja wenu ajisitiri.” (Abu Daawuud (4011). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abu Daawuud” (4011))

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24760/هل-تجوز-التسمية-بعبد-الستار-وعبد-الستير
  • Imechapishwa: 07/12/2024