Mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo mara kwa mara kuwaswalisha watu

Swali: Je, inafaa kwa mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo hovyo kuwaswalisha watu?

Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba haimpasi kwake kuwaswalisha watu. Aswali kama maamuma. Hata hivyo sitambui dalili ya wazi juu ya hili, kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru. Akiwaswalisha watu itasihi. Lakini kujiepusha na hilo huenda ni bora zaidi ili kuepuka makinzano ya maoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24755/هل-تجوز-امامة-صاحب-السلس
  • Imechapishwa: 06/12/2024