Mwenye mimba bora afunge au asifunge?


Swali: Mwanamke mjamzito akiambiwa na daktari mwaminifu kwamba kufunga kunaweza kumuathiri mtoto tumboni. Lakini hata hivyo taathira hii sio kubwa kwa sababu uzani wa mtoto tu ndio utapungua. Lakini baada ya kuzaliwa uzani wake utaongezeka kwa haraka – kwa idhini ya Allaah. Katika hali hii ni wajibu kwake kufunga au lililo bora kwake ni yeye kuacha kufunga kwa sababu ya mtoto?

Jibu: Ikiwa hakutomdhuru mtoto na hatohisi uzito wa kufunga, basi afunge. Kupungua uzani kwa mtoto inaweza kuwa ni jambo lenye manufaa kwake. Kwa sababu akipungua uzani wake atatoka kwa wepesi. Baada ya kuzaliwa atapewa chakula na uzani wake utaongezeka. Ama daktari akisema kuwa kunamdhuru kwa njia ya kwamba mtoto hapati chakula kupitia damu, mifupa na mishipa, katika hali hii usifunge. Au akawa anahisi uzito yeye. Kwa sababu wanawake wanatofautiana katika mimba zao. Jengine ni kwamba mimba ina hali tofauti mwanzoni mwake na mwishoni mwake. Hivyo pindi atapohisi uzito au kukakhofiwa juu ya mtoto basi asifunge.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1379
  • Imechapishwa: 03/12/2019