Mwenye kuzisahihisha Hadiyth hizi ni mwongo

Mwenye kusema kuwa Hadiyth zenye kusema kuwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf (Radhiya Allaahu ´anh) ataingia Pepo hali ya kutambaa na kwamba yeye ndiye Swahabah wa mwisho ambaye atayeingia, kwamba Abu Bakr alisema kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimweleza:

“Nilimuona Mola wangu kwa macho yangu.”

na kwamba alimwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhum):

“Nilimuona Mola wangu kwa moyo wangu.”

kuwa ni Swahiyh, ni mzushi na mwongo kwa mujibu wa wanazuoni wote. Mtu kama huyo anastahiki kutiwa adabu vikali.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar-ul-Fataawaa al-Miswriyyah (2/420)
  • taaliki: Imaam Badr-ud-Diyn Muhammad bin ´Aliy al-Hanbaliy al-Ba´liy