Swali: Wakati nilipokuwa katika umri mchanga nilikuwa nikizidisha kufanya maasi. Lakini hata hivyo sikuwa naacha mambo ambayo ni ya wajibu ya Uislamu. Mimi hivi sasa nimetubu kwa Allaah kutokamana na maasi yote kwa shakili ya jumla. Lakini nakosa ladha ya imani na nimekuwa ni mwenye kuishi hali ya kudangana na wasiwasi. Pindi ninapotoa shahaadah nahisi kuwa shahaadah yangu haifiki moyoni. Naogopa Allaah asije kuupiga muhuri moyo wangu.
Jibu: Tunakunasihi kumshukuru Allaah sana kutokana na yale aliyokutunuku katika kutubia. Fanya matendo mema mengi na mjengee dhana nzuri Mola Wako. Mtaja Allaah kwa wingi, soma Qur-aan kwa mazingatio, tangamana na watu wema na jiepushe na watu waovu. Pata bishara ya kheri na mwisho mwema. Baada ya kufanya niliyokutajia utapata – Allaah akitaka – ladha ya imani, ladha ya shahaadah mbili na matunda ya tawbah ya kweli. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ
“Tanabahi! Kwa kumdhukuru Allaah nyoyo hutulia!”[1]
وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
“Tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, mpate kufaulu.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake na tawbah inafuta yaliyokuwa kabla yake.”
“Mwenye kutubia kutokamana na dhambi ni kana ambaye hana dhambi.”
Mwenye kumtaja Allaah kwa wingi na akawa mkweli katika kutubia kwake basi atapata kufaulu, utulivu, moyo wenye raha na makosa yake yatafutwa. Allaah akuthibitishe juu ya uongofu na akutunuku kunyooka sawasawa.
[1] 13:28
[2] 24:31
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/57) https://binbaz.org.sa/fatwas/962/%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%83%D8%AB%D8%B1-%D9%85%D9%86-%D8%B0%D9%83%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87-%D8%A7%D8%B7%D9%85%D8%A7%D9%86-%D9%82%D9%84%D8%A8%D9%87-%D9%88%D8%A7%D8%B1%D8%AA%D8%A7%D8%AD-%D8%B6%D9%85%D9%8A%D8%B1%D9%87
- Imechapishwa: 10/12/2019
Swali: Wakati nilipokuwa katika umri mchanga nilikuwa nikizidisha kufanya maasi. Lakini hata hivyo sikuwa naacha mambo ambayo ni ya wajibu ya Uislamu. Mimi hivi sasa nimetubu kwa Allaah kutokamana na maasi yote kwa shakili ya jumla. Lakini nakosa ladha ya imani na nimekuwa ni mwenye kuishi hali ya kudangana na wasiwasi. Pindi ninapotoa shahaadah nahisi kuwa shahaadah yangu haifiki moyoni. Naogopa Allaah asije kuupiga muhuri moyo wangu.
Jibu: Tunakunasihi kumshukuru Allaah sana kutokana na yale aliyokutunuku katika kutubia. Fanya matendo mema mengi na mjengee dhana nzuri Mola Wako. Mtaja Allaah kwa wingi, soma Qur-aan kwa mazingatio, tangamana na watu wema na jiepushe na watu waovu. Pata bishara ya kheri na mwisho mwema. Baada ya kufanya niliyokutajia utapata – Allaah akitaka – ladha ya imani, ladha ya shahaadah mbili na matunda ya tawbah ya kweli. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ
“Tanabahi! Kwa kumdhukuru Allaah nyoyo hutulia!”[1]
وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
“Tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, mpate kufaulu.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake na tawbah inafuta yaliyokuwa kabla yake.”
“Mwenye kutubia kutokamana na dhambi ni kana ambaye hana dhambi.”
Mwenye kumtaja Allaah kwa wingi na akawa mkweli katika kutubia kwake basi atapata kufaulu, utulivu, moyo wenye raha na makosa yake yatafutwa. Allaah akuthibitishe juu ya uongofu na akutunuku kunyooka sawasawa.
[1] 13:28
[2] 24:31
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/57) https://binbaz.org.sa/fatwas/962/%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%83%D8%AB%D8%B1-%D9%85%D9%86-%D8%B0%D9%83%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87-%D8%A7%D8%B7%D9%85%D8%A7%D9%86-%D9%82%D9%84%D8%A8%D9%87-%D9%88%D8%A7%D8%B1%D8%AA%D8%A7%D8%AD-%D8%B6%D9%85%D9%8A%D8%B1%D9%87
Imechapishwa: 10/12/2019
https://firqatunnajia.com/mwenye-kumtaja-allaah-kwa-wingi-moyo-wake-hupata-utulivu-na-akahisi-raha-moyoni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)