Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa yule ambaye anataka kuhiji mwaka huu aswali swalah ya Istikhaarah?

Jibu: Ikiwa ni ile hajj ya wajibu haijuzu kwake kuswali swalah ya Istikhaarah. Kwa sababu ni lazima tu ahiji. Kwa sababu mtu anatakiwa kutekeleza faradhi haraka iwezekanavyo. Ama ikiwa ni hajj iliyopendekezwa, anaweza kumtaka Allaah ushauri kama ahiji mwaka huu au mwaka ujao. Kwa sababu kuhusiana na hajj iliyopendekezwa akitaka anaweza kuhiji mwaka huu, mwaka ujao au mwaka baada ya hapo. Lakini hajj ya wajibu asimtake Allaah ushauri. Kwa sababu Allaah ameshahukumu na kuwajibisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1396
  • Imechapishwa: 10/12/2019