Swali: Vipi mtu aliyelala na akakosa swalah ya usiku?

Jibu: Atailipa wakati wa mchana. Bora zaidi ni wakati wa Dhuhaa. Ikiwa atailipa baada ya adhuhuri hakuna tatizo. Lakini kama atailipa kabla ya jua kupinduka ni bora zaidi. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Atakayekosa sehemu yake ya usiku akaiswali mchana kabla ya swalah ya Dhuhr, atapata ujira kama kwamba ameswali usiku.”

au:

”… ataandikiwa kama aliyeiswali usiku.”

Hivyo swalah ambazo mtu amezikosa – kama sehemu yake ya Qur-aan – akiziswali wakati wa Dhuhaa inakuwa bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31183/حكم-القضاء-لمن-نام-عن-صلاة-الليل
  • Imechapishwa: 10/10/2025