Swali: Mtu amehiji na baada ya kumaliza kurusha vijiwe siku ya ´Iyd na siku ya 11, 12 na siku ya 13, akaenda Haram ambapo akatufu na akafanya Sa´y kwa ajili ya Hajj, kisha akatoka moja kwa moja bila kuaga hali ya kuamini kuwa inatosha kwa Twawaaf ya Hajj. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Wanazuoni wamesema wazi kuwa mtu akitufu mwisho wa usiku inamtosheleza badala ya Twawaaf ya kuaga. Ikiwa atachelewesha Twawaaf ya matembezi na akatufu baada ya kumaliza kurusha vijiwe vyote, kisha akasafiri papohapo, basi hilo linamtosheleza. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Asiondoke yeyote miongoni mwenu mpaka mwisho wa jambo lake uwe ni Nyumba tukufu.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Hadiyth ya pili, kupitia kwa Ibn ´Abbaas, kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha watu kuwa mwisho wa jambo lao uwe ni Nyumba Tukufu, isipokuwa aliwafanyia wepesi wanawake walio na hedhi. Ikiwa mwisho wa jambo lake ni Nyumba Tukufu basi hakuna tatizo. Mwenye hedhi hana wajibu wa kuaga, na mwanamke aliye na damu ya uzazi vilevile hana wajibu wa kuaga. Lakini ikiwa yeye mwanamume ametufu au mwanamke ambaye si mwenye hedhi wala damu ya uzazi akatufu wakati wa kutoka, Twawaaf ya kutoka, Twawaaf-ul-Ifaadhwah, Twawaaf ya Hajj, hata ikiwa imeambatana na Sa´y basi yanamtosheleza na hapaswi kuaga tena. Akifanya Twawaaf ya kuaga baada ya Twawaaf ya Hajj, basi huo ni ukamilifu na bora zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1096/من-ترك-طواف-الوداع-للحاج
- Imechapishwa: 29/01/2026
Swali: Mtu amehiji na baada ya kumaliza kurusha vijiwe siku ya ´Iyd na siku ya 11, 12 na siku ya 13, akaenda Haram ambapo akatufu na akafanya Sa´y kwa ajili ya Hajj, kisha akatoka moja kwa moja bila kuaga hali ya kuamini kuwa inatosha kwa Twawaaf ya Hajj. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Wanazuoni wamesema wazi kuwa mtu akitufu mwisho wa usiku inamtosheleza badala ya Twawaaf ya kuaga. Ikiwa atachelewesha Twawaaf ya matembezi na akatufu baada ya kumaliza kurusha vijiwe vyote, kisha akasafiri papohapo, basi hilo linamtosheleza. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Asiondoke yeyote miongoni mwenu mpaka mwisho wa jambo lake uwe ni Nyumba tukufu.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Hadiyth ya pili, kupitia kwa Ibn ´Abbaas, kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha watu kuwa mwisho wa jambo lao uwe ni Nyumba Tukufu, isipokuwa aliwafanyia wepesi wanawake walio na hedhi. Ikiwa mwisho wa jambo lake ni Nyumba Tukufu basi hakuna tatizo. Mwenye hedhi hana wajibu wa kuaga, na mwanamke aliye na damu ya uzazi vilevile hana wajibu wa kuaga. Lakini ikiwa yeye mwanamume ametufu au mwanamke ambaye si mwenye hedhi wala damu ya uzazi akatufu wakati wa kutoka, Twawaaf ya kutoka, Twawaaf-ul-Ifaadhwah, Twawaaf ya Hajj, hata ikiwa imeambatana na Sa´y basi yanamtosheleza na hapaswi kuaga tena. Akifanya Twawaaf ya kuaga baada ya Twawaaf ya Hajj, basi huo ni ukamilifu na bora zaidi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1096/من-ترك-طواف-الوداع-للحاج
Imechapishwa: 29/01/2026
https://firqatunnajia.com/mwenye-kuacha-twawaaf-ya-kuaga-katika-hajj/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket