Swali: Mtu anayekula ribaa pamoja na hivyo ni mwenye kuhifadhi swalah ya mkusanyiko, anasimama usiku, anaadhini kwa ajili ya swalah ya Fajr na anafanya matendo mema mbalimbali. Lakini pamoja na haya yote anakula ribaa. Anaponasihiwa katika hilo anasema kuwa kwamba jambo hilo ni uchumi wa ulimwenguni na kwamba wako katika wanachuoni waliohalalisha jambo hilo na akakasirika kwa ajili ya hilo. Je, mtu huyu yanaporomoka matendo yake yote kwa kitendo hichi?

Jibu: Kuna mambo ambayo wanachuoni wametofautiana katika ribaa. Ikiwa jambo hili ni miongoni mwa mambo ambayo wanachuoni wametofautiana, mtu huyu hakuufuru. Lakini hata hivyo anatiwa kwenye makosa na kusema kwamba amekosea na amepotea. Ama ikiwa jambo hilo ni miongoni mwa yale mambo ambayo wanachuoni wana kauli moja, mtu huyu anakufuru. Akisema kuwa ribaa ya kipindi cha kikafiri ni halali na anakusudia ile nyongeza, hili ni jambo ambalo wanachuoni wana kauli moja juu ya uharamu wake. Hivyo mtu huyu anaritadi kutoka katika Uislamu. Masuala ya ribaa yapo mambo ambayo wanachuoni wana kauli moja juu yake. Kama mfano wa ribaa ya kipindi cha kikafiri. Kuhusu baadhi ya mambo ambayo kuna tofauti juu yake, mtu huyu anatiwa kwenye makosa akiitumia na wala hakufurishwi. Hata kama atakula ribaa ambayo kuna maafikiano juu yake na asihalalishe, hakufuru midhali anaonelea kuwa ribaa ni haramu. Kama anaamini kuwa ribaa ni haramu lakini hata hivyo akaila, huyu anazingatiwa kuwa ametenda dhambi kubwa na juu yake kuna matishio. Lakini hata hivyo hakufuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
  • Imechapishwa: 29/11/2018