Swali: Je, ni bora kwa muislamu wakati anapoyatembelea makaburi kuelekea Qiblah na kumwombea du´aa maiti au amwelekee yule maiti na kumuombea du´aa?

Jibu: Kama ambavo unaposimama mbele ya mtu aliye hai; amwelekee yule maiti. Unapotaka kumsalimia au kula pamoja na muislamu aliye hai, unamwelekea. Kadhalika anatakiwa kumwelekea yule maiti, amsalimie na kumwombea du´aa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 19/07/2024