Mwanaume kuwatazama wanawake kama hakuna mashaka?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanaume kumtazama wanawake bila ya mashaka?

Jibu: Ni lazima kushusha macho. Lakini ni sawa akihitajia kufanya hivo kama vile kutafuta kilichopotea, msichana wake aliyepotea, kuna watu wamegunduliwa na kijakazi wake aliyepotea. Hapana vibaya haja ikipelekea kufanya hivo kama vile msichana wake amepotea, mke wake amepotea, kijakazi wake amepotea katika nchi ambayo hawajisitiri. Katika hali hiyo inafaa kwake kutazama… pengine ni msichana wake, mke wake au kijakazi wake.

´Allaamah ar-Raajihiy anauliza: Mshereheshaji anasema kuwa mtunzi kwa udhahiri wa kichwa cha khabari ni kwamba anaonelea kufaa mwanamke kumtazama mwanaume wa kando naye na si kinyume chake.

Ibn Baaz: Inatosha kama ni pasi na mashaka. Bila ya mashaka. Ni kama mfano wa kumtazama ami au akatazama kwa ajili ya utambulisho ili kujua kama mtu huyo ni kaka yake, baba yake au mume wake. Lakini ikiwa kuna mashaka hilo ndio linalokatazwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23919/هل-يجوز-نظر-الرجال-للنساء-بدون-ريبة
  • Imechapishwa: 05/06/2024