Swali: Imekuja katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwanaume asikusanye kati ya mwanamke na shangazi yake wala kati ya mwanamke na mama yake mdogo.”
Je, inajuzu kwa mwanaume kujifunua mbele ya shangazi au mama mdogo wa mke wake? Ikiwa haijuzu, ni ipi maana ya Hadiyth hii?
Jibu: Hadiyth hii maana yake ni kuwa haijuzu kumkusanya mke pamoja na shangazi yake au pamoja na mama yake mdogo katika ndoa moja. Kwa maana nyingine ni kwamba haijuzu kwake kumuoa Faatwimah na pamoja na shangazi yake aitwaye Khadiyjah au mama yake mdogo. Haijuzu kuwakusanya wawili hao katika ndoa moja, ni mamoja awe mkubwa kisha mdogo au mdogo kisha mkubwa. Ikiwa ana mke Faatwimah na akawa na shangazi au mama mkubwa au mdogo, basi asiwaoe wote wawili pamoja. Kadhalika ikiwa ana binti ya kaka au binti ya dada yake, basi asiwaoe wote wawili pamoja.
Ama wasichana wa baba mkubwa au baba mdogo au wasichana wa shangazi, hakuna tatizo; anaweza kuwakusanya katika ndoa. Lakini mwanamke na shangazi yake au mwanamke na mama yake mdogo, haijuzu kuwakusanya katika ndoa moja.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31008/حكم-جمع-الرجل-بين-المراة-وعمتها-او-خالتها
- Imechapishwa: 21/09/2025
Swali: Imekuja katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwanaume asikusanye kati ya mwanamke na shangazi yake wala kati ya mwanamke na mama yake mdogo.”
Je, inajuzu kwa mwanaume kujifunua mbele ya shangazi au mama mdogo wa mke wake? Ikiwa haijuzu, ni ipi maana ya Hadiyth hii?
Jibu: Hadiyth hii maana yake ni kuwa haijuzu kumkusanya mke pamoja na shangazi yake au pamoja na mama yake mdogo katika ndoa moja. Kwa maana nyingine ni kwamba haijuzu kwake kumuoa Faatwimah na pamoja na shangazi yake aitwaye Khadiyjah au mama yake mdogo. Haijuzu kuwakusanya wawili hao katika ndoa moja, ni mamoja awe mkubwa kisha mdogo au mdogo kisha mkubwa. Ikiwa ana mke Faatwimah na akawa na shangazi au mama mkubwa au mdogo, basi asiwaoe wote wawili pamoja. Kadhalika ikiwa ana binti ya kaka au binti ya dada yake, basi asiwaoe wote wawili pamoja.
Ama wasichana wa baba mkubwa au baba mdogo au wasichana wa shangazi, hakuna tatizo; anaweza kuwakusanya katika ndoa. Lakini mwanamke na shangazi yake au mwanamke na mama yake mdogo, haijuzu kuwakusanya katika ndoa moja.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31008/حكم-جمع-الرجل-بين-المراة-وعمتها-او-خالتها
Imechapishwa: 21/09/2025
https://firqatunnajia.com/mwanaume-kukusanya-baina-ya-mwanamke-na-shangazi-au-mama-yake-mkubwa-au-mdogo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket