Swali: Kuna mtu alimtaliki mke wake mara tatu au mara nne akiwa na hasira. Hivi sasa anaishi pamoja naye. Ni ipi hukumu ya kitendo hicho? Ni kipi kinachomlazimu mwanamke?
Jibu: Ikiwa alikasirika sana kiasi cha kwamba hajui kile anachokisema, talaka haikupita. Kwa sababu anazingatiwa ni kama mwendawazimu. Hadiyth inasema:
“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”[1]
Anazingatiwa kama mwendawazimu. Lakini kama alikuwa amekasirika kawaida, talaka nyingi zinatokea katika hali ya ghadhabu. Ikiwa alikuwa anajua na kuelewa kile anachokisema, talaka imepita. Ikiwa alikuwa anajua na anatambua kile alichokuwa anakisema, maana yake ni kwamba anazini na mwanamke huyo na anafanya naye jambo la haramu. Ikiwa ameshamwacha mara tatu, basi si halali kwake mpaka aolewe na mume mwingine. Hapa ni pale ambapo alikuwa amekasirika na anajua kile anachokisema. Hata hivyo hazipiti ikiwa ni moja katika zile aina tatu, au ni aina tatu zote, alikuwa katika hali ya hasira sana na hatambui kile anachokisema, kwa sababu alikuwa kama mwendawazimu.
[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 430-431
- Imechapishwa: 20/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket