Mwanamke mwenye talaka ya tatu kutoka nyumbani

Swali: Mwanamke huyu anasema kuwa yeye ametalikiwa talaka ya tatu. Je, inajuzu kwake kutoka na familia yake kwa ajili ya haja zake na kwenda kutembea au ni lazima kwake kubaki nyumbani?

Jibu: Hapana. Talaka ya tatu [ya mume] aliehai, habaki nyumbani kwake. Anaenda katika haja zake. Hili linahusiana na aliyefiliwa, yeye ndiye anatakiwa kubaki nyumbani. Ama talaka ya tatu ya mwanaume aliehai, miongoni mwa sharti za eda yake sio kubakia nyumbani.

Check Also

Kumjamii mke ndani ya eda ndio kumrejea     

Swali: Mtu akimtaliki mkewe na ndani ya eda akamwingilia pasi na kukusudia kwa kufanya hivo …