Mwanamke mwema yuko huru katika mali yake

Swali: Mwanamke huyu anauliza kama ni wajibu kwake kumwambia mume wake kuhusu mali yake maalum jinsi anavyoitoa au aitoe pasi na kumwambia?

Jibu: Amehadithia Ibn Jariyr (Rahimahu Allaah) juu ya kukubaliana kwa wanachuoni ya kwamba mwanamke mwema yuko huru kuitumia mali yake. Kwa hivyo sio lazima kumwambia. Yuko huru. Lakini hakuna neno ukamshauri na kumshirikisha, hili halina neno ukamwambia “Nimefanya kadhaa na kadhaa”. Lakini akiona kitu kutoka kwake kisichoenda sawa, kama israfu, ubadhirifu na kadhalika ambapo [mume wake] akamnasihi, basi ni wajibu kwake [mke] kumsikiliza na kumtii.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/3766
  • Imechapishwa: 20/09/2020