Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini hali ya kuwa amejisitiri, amejiheshimu, hakujitia manukato na wala haonyeshi manukato na yeye amefanya hivo kwa kutaka uso wa Allaah mbali na kwamba mume wake haridhii jambo hilo?
Jibu: Inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini akiwa amejisitiri na hakujitia manukato. Haifai kwa mumewe kumzuia kutokamana na hilo akilazimiana na zile adabu za ki-Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah.”[1]
“Mmoja wenu akiombwa idhini na mke wake ya kwenda msikitini basi asimkatalie.”[2]
Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.
Akitoka nje kwa staha na pasi na manukato hapana neno ijapo mume wake si mwenye kuridhia kutokana na Hadiyth mbili zilizotajwa. Na akiswali nyumbani kwake na asitoke kwa sababu ya kuitakasa nafsi yake na kujiepusha na sababu za fitina ndio bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah na nyumba zao ni bora kwao.”[3]
[1] al-Bukhaariy (849) na Muslim (668) na tamko ni lake.
[2] Ahmad (4328), al-Bukhaariy (4837) na Muslim (666).
[3] Ahmad (5211) na Abu Daawuud (480).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/79)
- Imechapishwa: 20/11/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
84. Ndio maana ikakatazwa mwanamke kutoka amejipaka manukato
Sababu ya makatazo iko wazi kwa sababu harufu nzuri na manukato yanaamsha matamanio. Wanazuoni wameimbatanisha dhambi hiyo na madhambi kama ya mavazi ya marembo, vito vinavyoonekana na kuchanganyika na wanamme[1]. Ibn Daqiyq-il-´Iyd amesema: ”Kunafahamisha kuwa ni haramu kwa wanawake wanaotaka kwenda kuswali msikitini kujitia manukato, kwa sababu kunahamasisha matamanio ya…
In "5. Sharti ya tano ya jilbaab"
29. Adabu za kuzingatia wakati mwanamke anatoka kwenda msikitini
6 - Akitoka kwenda msikitini basi ni lazima kuchunga adabu zifuatazo: 1 - Awe ni mwenye kujisitiri kwa mavazi na Hijaab kamilifu. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema: “Wanawake walikuwa wakiswali pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kisha wanaondoka zao hali ya kujigubika mavazi yao. Hakuna yeyote…
In "05. Sura ya tano: Hukumu zinazohusu swalah ya mwanamke"
Akifunika mwili mzima anaruhusiwa kwenda msikitini
Swali: Msichana mdogo ambaye amevaa Hijaab na ambaye ameshikamana na vazi la Kiislamu lililowekwa katika Shari´ah na anausitiri mwili wake mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono. Je, anaruhusiwa akitaka kuswali kila nyakati ya swalah msikitini kufanya hivo? Je, anaruhusiwa daima kwenda na mume wake? Jibu: Hapana vibaya kwa mwanamke…
In "Niqaab, Burqu´ na vifuniko vya mikono"