Mwanamke hatoki ndani ya eda mpaka aoge baada ya hedhi ya tatu?

Swali 555: Nilimuuliza Shaykh wetu kuhusu mwenye kusema kuwa mwanamke aliyeachika hatoki ndani ya eda mpaka pale atakapooga baada ya hedhi ya tatu?

Jibu: Alitaja maelezo fulani, kisha akasema: Sahihi ni kuwa inafaa kwake kutoka katika eda hata kama hajakoga baada ya kusafika, kwa sababu inajuzu kumpa talaka baada ya kutwaharika kabla ya kuoga na vilevile swawm yake ni sahihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 189
  • Imechapishwa: 11/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´