Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke asiyeoga josho la janaba ilihali anajua kuwa ni lazima?

Jibu: Anapata dhambi na amefanya haramu. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا

“Mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni.”[1]

Ni wajibu kwa kila muislamu kuharakisha kujisafisha unapofika wakati wa swalah. Ikiwa wamefanya tendo la ndoa mwanzoni mwa usiku inafaa wakaenda kuoga pamoja au kila mmoja akaoga kivyake. Inafaa vilevile na hapana vibaya kuiahirisha mpaka kabla ya Fajr. Wanaweza vilevile wakatawadha wudhuu´ wa swalah kisha wakalala. Hapana vibaya kufanya hivo. Lakini unapofika wakati wa swalah ni lazima kwake kuoga na kuswali. Na unapofika wakati wa swalah na asioge na kuswali anazingatiwa kuwa ni kafiri.

[1] 05:06

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 441
  • Imechapishwa: 14/07/2025