Mwanamke anayekaa eda kuvua vito vyake

Swali: Je, vito vya mwanamke aliyefiwa vinaondolewa, hata kama kuna uzito au tabu katika kuviondoa? Je, kipindi cha eda kinamuhusu pia mwanamke mzee sana?

Jibu: Ndiyo, eda inamuhusu msichana mdogo na pia mwanamke mzee, wote wawili wanawajibika kukaa eda. Inamuhusu mwanamke aliyeingiliwa na mumewe na pia ambaye bado hajaingiliwa. Hata kama mume alimuoa mwanamke na akafa kabla ya kumwingilia, basi mwanamke huyo analazimika kukaa eda. Hili ni tofauti na talaka, kwani mwanamke aliyetalikiwa kabla ya kuingiliwa hana ukaaji eda. Lakini mwanamke ambaye mumewe amefariki, hata kama hajaingiliwa, anawajibika kukaa eda na anayo haki ya kurithi. Kwa hiyo mwanamke mzee na kijana wote ni sawa katika ulazima wa kukaa eda. Pia ikiwa mwanamke ana mapambo au vito, vinatakiwa kuvuliwa. Hata kama ni bangili na imebana mkononi, hukatwa ili itoke, haitakiwi kubaki juu ya mkono wake wakati wa kipindi cha ukaaji eda.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1140/حكم-الاحداد-للكبيرة-والحلية-التي-يشق-نزعها
  • Imechapishwa: 31/01/2026