Swali: Nimesoma katika jarida la ”al-Muslimuun” makala ya Muhammad al-Ghazaaliy anayesema humo kwamba hakuna kizuizi kwa mwanamke kuchukua nafasi ya uhakimu. Ametaja kuwa ´Umar alimpa ash-Shifaa´ mwanamke wa koo yake jukumu fulani. Anasema: ”Ninapowasilisha Uislamu katika nchi nyingine, basi nataka nisione tabia inayobadilishwa katika nchi hii na kwamba baadhi ya wanazuoni wetu wanaona hakuna tatizo katika hilo.”
Jibu: Huu ni msimamo dhaifu. Kile wanachoona jopo kubwa la wanazuoni ni kwamba haijuzu mwanamke kupewa jukumu hilo. Yeye anapewa yale yanayomfaa kama kusimamia shule, kufundisha tiba na yaliyo mfano wa hayo. Ama nafasi ya uhakimu, haichukuliwi isipokuwa na wanaume. Hivi ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hawatafaulu watu ambao wamemtawalisha jambo lao mwanamke.”
Hii ni Hadiyth adhimu. Ameipokea al-Bukhaariy na wengineo.
Kuhusu masimulizi yaliyopokelewa kutoma kwa ´Umar, hatuijui usahihi wake na wala hatujui hata chanzo chake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1239/الرد-على-من-اجاز-تولية-المراة-للقضاء
- Imechapishwa: 14/02/2026
Swali: Nimesoma katika jarida la ”al-Muslimuun” makala ya Muhammad al-Ghazaaliy anayesema humo kwamba hakuna kizuizi kwa mwanamke kuchukua nafasi ya uhakimu. Ametaja kuwa ´Umar alimpa ash-Shifaa´ mwanamke wa koo yake jukumu fulani. Anasema: ”Ninapowasilisha Uislamu katika nchi nyingine, basi nataka nisione tabia inayobadilishwa katika nchi hii na kwamba baadhi ya wanazuoni wetu wanaona hakuna tatizo katika hilo.”
Jibu: Huu ni msimamo dhaifu. Kile wanachoona jopo kubwa la wanazuoni ni kwamba haijuzu mwanamke kupewa jukumu hilo. Yeye anapewa yale yanayomfaa kama kusimamia shule, kufundisha tiba na yaliyo mfano wa hayo. Ama nafasi ya uhakimu, haichukuliwi isipokuwa na wanaume. Hivi ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hawatafaulu watu ambao wamemtawalisha jambo lao mwanamke.”
Hii ni Hadiyth adhimu. Ameipokea al-Bukhaariy na wengineo.
Kuhusu masimulizi yaliyopokelewa kutoma kwa ´Umar, hatuijui usahihi wake na wala hatujui hata chanzo chake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1239/الرد-على-من-اجاز-تولية-المراة-للقضاء
Imechapishwa: 14/02/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-anaweza-kuwa-qaadhiy/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket