Mwanamke anataka arudishiwe zamu yake aliyokuwa ameipeana kwa wakewenza

Swali: Ikiwa mwanamume ameoa mke wa pili na yule mke wa kwanza akakataa kulala naye usiku au kukaa naye kisha baadaye akakubali. Je, mume ampe zamu yake?

Jibu: Amlazimishe mwanamke huyo.

Swali: Lakini ampe zamu yake au hakuna haja?

Jibu: Mwanamke huyo analazimika kunyenyekea hukumu ya Shari´ah na aridhie ugavi wa Allaah. Ni mamoja wake ni wawili, watatu au wanne. Mwanamke huyo akikataa hatopewa zamu. Haki yake itaanguka. Yeye ndiye ambaye amedondosha haki yake. Hatogawanyiwa chochote.

Swali: Akitoa zawadi ya siku yake kisha baadaye akaitaka?

Jibu: Anayo haki ya kuitaka tena. Amwambie ampe haki yake au amtaliki, kwa sababu pengine asiweze kusubiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23896/هل-للزوجة-طلب-استرجاع-حقها-الذي-اسقطته
  • Imechapishwa: 29/05/2024