Mwanamke anapaswa kuoga hata akipata hedhi kidogo tu

Swali: Ni kiwango gani kinachosamehewa katika hedhi?

Jibu: Hakuna kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuoga kwa aina zote. Kwa ajili hiyo mtunzi amezindua ya kwamba hakubaguliwi chochote. Bali ni wajibu kuoga kwa damu aina yote ingawa ni damu kidogo. Mwanamke mwenye hedhi analazimika kuoga. Kinachosamehewa ni damu kidogo inayotoka kwa mfano puani, kwenye meno na kwenye macho. Dama kama hiyo inayotoka kwenye majeraha ndio inayosamehewa kidogo. Ama kuhusu hedhi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuoga kwa aina zote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24692/هل-يعفى-عن-شيء-في-غسل-دم-الحيض
  • Imechapishwa: 27/11/2024