Swali: Mwanamke aliweka sharti kabla ya kufungwa ndoa kwamba mchumba wake asimtaliki ambapo mume akalikubali sharti hilo. Je, sharti hili ni sahihi? Je, mwanamke ana haki ya kushurutisha kuwa talaka iwe mikononi mwake?

Jibu: Sharti hili si sahihi. Mume ana haki ya kumtaliki mke wake wakati wowote atakapoona inafaa. Haijuzu kuweka sharti kwamba talaka iwe mikononi mwa mwanamke wala sharti kwamba asitaliki kabisa, kwa sababu huenda yakatokea mambo yatakayolazimisha talaka. Kwa hiyo ikiwa aliweka sharti kwamba hamtaliki, bado ana haki ya kumtaliki ikiwa kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Kwa sababu sharti hilo si sahihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/46)
  • Imechapishwa: 19/03/2026