Swali: Kuna mwanamke wa kimarekani ambaye amehajiri Saudi Arabia peke yake na wakati mwingine anahitajia kusafiri kwenda nchi za nje kwa ajili ya visa na mambo mengine mfano wake. Afanye nini?

Jibu: Afanye nini kama amelazimika kufanya hivo? Asafiri, kwa sababu amelazimika. Vivyo hivyo inafaa kwa mwanamke kuhajiri bila Mahram, kama walivofanya baadhi ya Maswahabah wa kike.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 18/02/2022