Swali: Je, inajuzu kumwambia mwanachuoni kwamba Allaah amekufanya uwe kimbilio la waislamu na hifadhi ya waumini?

Jibu: Maana yake ni sahihi. Maana yake ni kuwa ni kimbilio kwao katika kupata haki zao kupitia mahakama za Kishari´ah au kupitia utawala, ambapo watu wanamkimbilia kwake ili awasaidie kupata haki zao. Hii ni maana sahihi. Ni du´aa njema kwa mtawala kwamba Allaah amfanye awe mwenye kufanikiwa na Allaah amsaidie katika kutekeleza mahitaji ya waislamu na kwamba pale wanapomkimbilia awatimizie wanayoyataka katika kusimamisha adhabu za Kishari´ah, kuondoa dhuluma, kurudisha haki na mambo mengine kama hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31396/ما-حكم-قول-قد-اقامكم-الله-مفزعا-للمسلمين
  • Imechapishwa: 17/10/2025