Swali: Katika baadhi ya nchi za Kiislamu watu hutengeneza chakula wanachokiita swadaqah kwa ajili ya maiti. Je, inajuzu kula chakula hicho?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba yale yanayozoeleka katika baadhi ya nchi kuhusu kufanya maombolezo na kutengeneza chakula kinachoitwa ”swadaqah ya maiti”, iwe ni siku ya kufa kwake, siku ya nne, ya saba au ya arobaini, yote hayo ni Bid´ah. Haitakiwi kufanywa wala haifai kuitikia mwaliko, kwa sababu kuitikia mwaliko huo kunasaidia na kuhimiza Bid´ah. Kwa hiyo maombolezo haya ambayo hutengenezwa chakula katika siku maalum kwa ajili ya maiti, ni mamoja iwe ni siku ya kufa, siku ya saba, siku ya kumi au siku ya arobaini au hata ya mwaka mmoja, yote haya ni Bid´ah. Haifai kuyaendea wala kula chakula chake, kwa sababu kuyajibu kunahesabika kama aina ya kuhimiza na kuendeleza Bid´ah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1540/حكم-صناعة-الطعام-باسم-الصدقة-على-الميت
- Imechapishwa: 27/03/2026
Swali: Katika baadhi ya nchi za Kiislamu watu hutengeneza chakula wanachokiita swadaqah kwa ajili ya maiti. Je, inajuzu kula chakula hicho?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba yale yanayozoeleka katika baadhi ya nchi kuhusu kufanya maombolezo na kutengeneza chakula kinachoitwa ”swadaqah ya maiti”, iwe ni siku ya kufa kwake, siku ya nne, ya saba au ya arobaini, yote hayo ni Bid´ah. Haitakiwi kufanywa wala haifai kuitikia mwaliko, kwa sababu kuitikia mwaliko huo kunasaidia na kuhimiza Bid´ah. Kwa hiyo maombolezo haya ambayo hutengenezwa chakula katika siku maalum kwa ajili ya maiti, ni mamoja iwe ni siku ya kufa, siku ya saba, siku ya kumi au siku ya arobaini au hata ya mwaka mmoja, yote haya ni Bid´ah. Haifai kuyaendea wala kula chakula chake, kwa sababu kuyajibu kunahesabika kama aina ya kuhimiza na kuendeleza Bid´ah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1540/حكم-صناعة-الطعام-باسم-الصدقة-على-الميت
Imechapishwa: 27/03/2026
https://firqatunnajia.com/mwaliko-wa-chakula-cha-maiti/