Swali: Kuna wajibu gani kwa mzazi katika kutoa kwake zawadi au kutoa mali kwa watoto wake ikiwa wamo wa kiume na wa kike? Je, inampasa kumpa msichana nusu ya anachompa mvulana?
Jibu: Wajibu ni uadilifu, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mcheni Allaah na fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu.”
Ni lazima awalinganishe; mwana wa kiume apewe sawa na sehemu ya wasichana wawili, kama katika mirathi. Akimpa mvulana 1000, basi ampe msichana 500. Lazima kuwe na uadilifu baina yao, isipokuwa tu kama wote ni watu wazima wenye ufahamu na wamekubali kwa moyo mmoja ruhusa ya mmoja kupewa zaidi. Katika hali hiyo hapana tatizo. Lakini kama bado hawajakomaa kifikra, hapana, ni lazima atende haki. Awalinganishe wote. Asimpe huyu na kumuacha huyu. Mtoto wa kike anapata nusu ya mtoto wa kiume hata kama ameolewa. Ni lazima awalinganishe yeye na ndugu zake. Asidhulumu. Afanye uadilifu kwa wote. Mtume amesema:

Swali: Je, akimnunulia mtoto gari au ardhi anatakiwa kufanya hivyohivyo kwa ndugu zake wengine?
Jibu: Gari au kitu kingine, isipokuwa kama kimeandikwa kwa jina la mzazi na kimetolewa tu kama dhamana ya kutumia kwenda shule na kurudi, si zawadi. Hapo hakuna tatizo. Lakini kama ni zawadi ya kumiliki, basi hapaswi kumpa mmoja bila wengine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31707/هل-يلزم-في-اعطية-الوالد-ان-تكون-وفق-الميراث
- Imechapishwa: 02/12/2025
Swali: Kuna wajibu gani kwa mzazi katika kutoa kwake zawadi au kutoa mali kwa watoto wake ikiwa wamo wa kiume na wa kike? Je, inampasa kumpa msichana nusu ya anachompa mvulana?
Jibu: Wajibu ni uadilifu, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mcheni Allaah na fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu.”
Ni lazima awalinganishe; mwana wa kiume apewe sawa na sehemu ya wasichana wawili, kama katika mirathi. Akimpa mvulana 1000, basi ampe msichana 500. Lazima kuwe na uadilifu baina yao, isipokuwa tu kama wote ni watu wazima wenye ufahamu na wamekubali kwa moyo mmoja ruhusa ya mmoja kupewa zaidi. Katika hali hiyo hapana tatizo. Lakini kama bado hawajakomaa kifikra, hapana, ni lazima atende haki. Awalinganishe wote. Asimpe huyu na kumuacha huyu. Mtoto wa kike anapata nusu ya mtoto wa kiume hata kama ameolewa. Ni lazima awalinganishe yeye na ndugu zake. Asidhulumu. Afanye uadilifu kwa wote. Mtume amesema:
”Mcheni Allaah na fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu.”
Swali: Je, akimnunulia mtoto gari au ardhi anatakiwa kufanya hivyohivyo kwa ndugu zake wengine?
Jibu: Gari au kitu kingine, isipokuwa kama kimeandikwa kwa jina la mzazi na kimetolewa tu kama dhamana ya kutumia kwenda shule na kurudi, si zawadi. Hapo hakuna tatizo. Lakini kama ni zawadi ya kumiliki, basi hapaswi kumpa mmoja bila wengine.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31707/هل-يلزم-في-اعطية-الوالد-ان-تكون-وفق-الميراث
Imechapishwa: 02/12/2025
https://firqatunnajia.com/mvulana-anapata-sawa-na-sehemu-ya-wasichana-wawili-katika-zawadi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket