Muuzaji anamshurutishia mnunuzi asiuze kile alichonunua

Swali: Nilinunua ardhi kutoka kwa ndugu yangu mmoja ambaye akaniwekea sharti kwamba nisiiuze. Je, sharti hii ni sahihi?

Jibu: Muuzaji akimuwekea sharti mnunuzi kwamba asimuuzie kile alichomuuzia, sharti hii inapingana na mkataba. Kwa sababu biashara inapelekea yule mnunuzi ndiye anakuwa mmiliki na ana haki ya kuiendesha vile anavotaka. Hiki ni kikwazo kumwambia kwamba usiiuze. Lakini ikiwa yule muuzaji ana sababu ya yule mnunuzi asiiuze, basi sharti ni sahihi. Mtu ana mtumwa anayemmiliki na kwake anamuona ni mwenye thamani. Akaja rafiki yake na kumuomba amuuzie mtumwa huyo ambapo akamjibu kwamba mtumwa huyo kwake ni mwenye thamani na hapendelei kumuuza. Akamuomba mara ya pili ambapo akamjibu kwamba hapendelei kumuuza isipokuwa kwa sharti kama hatomuuzia yeyote na kwamba pindi atapotaka kumuuza basi amuuzie yeye huyohuyo. Hapo sharti hiyo itakuwa ni yenye kufaa kwa kuwa ina lengo sahihi. Mfano mwingine mtu yuko na ng´ombe na akamuuzia mtu kwa sharti asimuuzie mtu fulani kwa sababu mtu huyo kwa mfano huwatesa ng´ombe, sharti hii ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1297
  • Imechapishwa: 18/10/2019