Mwenye kutaka kupotosha dalili juu ya kuonekana kwa Allaah Aakhirah basi anawafungulia mlango wakanamungu Baatwiniyyah. Watu hawa wamefasiri kimakosa maandiko kuhusu kufufuliwa, Pepo, Moto na hesabu na badala yake wakasema Pepo na Moto, al-Jannah wan-Naar, maana yake ni majazi. Wakati Mu´tazilah na wanafalsafa walipowaambia kuwa maandiko haya ya kufufuliwa yamethibiti na Pepo na Moto ni kitu sahihi kwa dalili zenye kukata mashauri kabisa. Baatwiniyyah na wao wakawaambia mbona na nyinyi mmekanusha maandiko ya kuhusu kuonekana kwa Allaah Aakhirah ilihali na yenyewe pia yemethibiti na maana yake imethibiti! Ni kipi chenye kuwajuzisihia nyinyi kupindisha [Ta´wiyl] maandiko ya sifa na isijuzu kwetu na sisi kupindisha maandiko ya kuhusu kufufuliwa na Pepo na Moto? Hivyo wakawa wamewafungulia mlango wakanamungu wa kufanya Ta´wiyl.
Vivyo hivyo ndivyo walivofanya mayahudi na manaswara kwa maandiko ya Tawrat na Injiyl. Allaah ametutahadharisha kufanya kama wao. Lakini pamoja na hivyo watu wa batili hawataki jengine isipokuwa kufuata njia yao.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/274-275)
- Imechapishwa: 21/05/2020
Mwenye kutaka kupotosha dalili juu ya kuonekana kwa Allaah Aakhirah basi anawafungulia mlango wakanamungu Baatwiniyyah. Watu hawa wamefasiri kimakosa maandiko kuhusu kufufuliwa, Pepo, Moto na hesabu na badala yake wakasema Pepo na Moto, al-Jannah wan-Naar, maana yake ni majazi. Wakati Mu´tazilah na wanafalsafa walipowaambia kuwa maandiko haya ya kufufuliwa yamethibiti na Pepo na Moto ni kitu sahihi kwa dalili zenye kukata mashauri kabisa. Baatwiniyyah na wao wakawaambia mbona na nyinyi mmekanusha maandiko ya kuhusu kuonekana kwa Allaah Aakhirah ilihali na yenyewe pia yemethibiti na maana yake imethibiti! Ni kipi chenye kuwajuzisihia nyinyi kupindisha [Ta´wiyl] maandiko ya sifa na isijuzu kwetu na sisi kupindisha maandiko ya kuhusu kufufuliwa na Pepo na Moto? Hivyo wakawa wamewafungulia mlango wakanamungu wa kufanya Ta´wiyl.
Vivyo hivyo ndivyo walivofanya mayahudi na manaswara kwa maandiko ya Tawrat na Injiyl. Allaah ametutahadharisha kufanya kama wao. Lakini pamoja na hivyo watu wa batili hawataki jengine isipokuwa kufuata njia yao.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/274-275)
Imechapishwa: 21/05/2020
https://firqatunnajia.com/mutazilah-ndio-wamewafungulia-mlango-wa-tawiyl-baatwiniyyah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)