Mume wa binti ni katika Mahram

Swali: Kuna mwanamke mwenye binti aliyeolewa. Mwanamke huyu anajisitiri mbele ya mume wa binti yake na wala hali naye chakula na hata siku za sherehe hamsalimii. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Mume wa binti ni katika Mahram kwa mama yake. Allaah (Subhaanah) amesema wakati alipokuwa akiwabaianishia wanawake wanaoharamika:

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ

“Mmeharamishiwa [kuwaoa] mama zenu na wasichana wenu na dada zenu na shangazi zenu na makhalati wenu na wasichana wa kaka na wasichana wa dada na mama zenu ambao wamekunyonyesheni na ndugu zenu kwa kunyonya na mama wa wake zenu… “ (04:23)

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/26)
  • Imechapishwa: 18/03/2026