Mume usifanye uzazi wa mpango bila ya idhini ya mke II

Swali: Hadiyth dhaifu kuhusu kuchomoa kabla ya kumwaga inakataza au inajuzisha?

Jibu: Hadiyth inayosema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkataza mwanaume kuchomoa kabla ya kumwaga kwa mwanamke muungwana isipokuwa baada ya idhini yake. Ameipokea Ahmad na katika cheni ya wapokezi kuna bwana asiyetambulika. Ndani yake kuna makatazo ya kuchomoa kabla ya kumwaga kwa mwanamke muungwana isipokuwa kwa idhini yake. Hata hivyo maana yake ni sahihi kwa upande wa maana. Kwa sababu mwanamke anayo haki ya kupata watoto. Ni wenye kushirikiana katika watoto.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23894/الحكم-على-حديث-النهى-عن-العزل-الا-باذن
  • Imechapishwa: 28/05/2024