Swali: Je, inafaa kwa mume kuchelewesha kulipa swawm?

Jibu: Kama ilivyotangulia. Haki ya Allaah ni yenye kutangulizwa. Deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa. Kuhusu kulipwa hapana. Deni la Ramadhaan linaweza kucheleweshwa mpaka katika Sha´baan, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth ya ´Aaishah. Kuhusu kafara za wajibu zinatekelezwa upesi na vilevile nadhiri za wajibu. Hata hivyo hapana vibaya inapokuja katika kulipa deni la Ramadhaan. ´Aaishah amesema:

“Nilikuwa na deni la swawm ya Ramadhaan na siwezi kuilipa isipokuwa katika Sha´baan.”[1]

Kwa sababu hapa kuna wasaa.

[1] al-Bukhaariy (1950) na Muslim (1146).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23879/هل-للزوج-الزام-زوجته-بتاخير-القضاء
  • Imechapishwa: 24/05/2024