Swali: Ipi hukumu ya mwenye kunuia kumtaliki mke wake na akachelewesha kufanya hivyo?
Jibu: Mwanaume akinuia kumtaliki mke wake kisha akaacha hilo na asifanye kitu, Talaka haipiti. Nia haifanyi Talaka kupita. Kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu yanayohadithia nafsi zao maadamu hawajayafanaya au kuyatamka.”
Maadamu hajayatamka na wala kuyafanya – kuandika hilo – isipokuwa kaweka nia tu, nia hii haipitishi chochote na mke atabaki katika asli yake. Talaka haipiti mpaka aandike Talaka au aitamke.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
- Imechapishwa: 18/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)