Mume anamzuia mke kwenda katika mikutano ya maasi

Swali: Baadhi ya jamaa wa mke wangu hukutana kila wiki kwa mmoja wao kwa ajili ya kuzungumza, kisha husikiliza nyimbo na kucheza. Mimi sasa nimemzuia mke wangu kwenda kwenye mikutano hiyo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Wewe una ujira mbele ya Allaah. Ikiwa mkutano huo unafanyika kwa ajili ya kucheza, kusikiliza nyimbo na mambo ya ufisadi, basi unamzuia mke wako kuhudhuria, jambo ambalo ni la haki na wewe una ujira kwa kufanya hivyo. Lakini ikiwa mikutano hiyo ni ya majirani au jamaa juu ya kheri na mazungumzo yanayoruhusiwa na yasiyo na mambo yaliyokatazwa, basi hakuna kosa kwake kuwatembelea majirani au kuhudhuria mikutano hiyo. Lakini ikiwa mikutano hiyo inahusisha nyimbo, ala za muziki na mambo yanayomchukiza Allaah, basi una haki kamili ya kumzuia na wewe una ujira kwa hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1747/حكم-حضور-الزوجة-للاجتماعات-العاىلية-التي-تصاحبها-اغاني-ولهو
  • Imechapishwa: 27/12/2025