Mume amejua kuwa jimaa wakati wa swawm inafunguza baada ya mkewe kufariki

Swali: Mwanaume alimjamii mke wake mchana wa Ramadhaan na alikuwa ni mjinga, lakini alipofariki akaijua hukumu baada ya mkewe kufa. Je, amfungie au atoe kafara?

Jibu: Allaah amjaze kheri iwapo atamtolea kafara. Atawalisha chakula masikini sitini na Allaah atamjaza kheri. Na akifunga ni sawa pia Allaah atamjaza kheri. Yote ni mazuri.

Swali: Je, afunge na kutoa kafara pia?

Jibu: Kinachomlazimu ni kufunga kama anaweza. Vinginevyo alishe chakula masikini sitini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24649/حكم-من-جامع-في-رمضان-جاهلا-وعلم-بالحكم-بعد-وفاة-زوجته
  • Imechapishwa: 21/11/2024