Swali: Unasemaje kuhusu suruwali za wanaume?
Jibu: Anayevaa suruwali anajifananisha na makafiri. Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao. Hii ni katika desturi iliwajia waislamu kutoka katika nchi za magharibi. Wamekuwa ni mikia ya wamagharibi. Wamechukua kivazi hichi cha suruwali zao. Wamechukua kashfa za wanawake. Ikiwa imekuwa ni jambo la kawaida kwa mwanamke kuonyesha uso wake, nywele zake na kifua chake, iwe pia ni jambo la kawaida kwa waislamu? Inaweza kusemwa vivyo hivyo kwa yale yote kutoka kwa manaswara kwa kutumia jina desturi.
Ni wajibu kwetu kuachana na desturi hizi mbaya na kushikamana na desturi za Kiislamu. Ikiwa watu hawa ni lazima kwao kuvaa suruwali basi wavae suruwali ambazo ni pana na za kuachia zinazofanana na mavazi ya waturuki na waislamu wasiokuwa waarabu. Hilo ni afadhali – Allaah akitaka – na inaweza kuwa inajuzu. Ama suruwali za kimagharibi zinazofichua misuli na viungo vingine vya mwili ni kujifananisha na makafiri:
“Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”[1]
Wanajifananisha na makafiri kwa suruwali zao, tai na kuacha kichwa wazi. Unakaribia kutoona tofauti kati ya muislamu na myahudi.
Wakati mayahudi na manaswara walipokuwa wanaishi chini ya utawala wa waislamu, walilazimishwa kuwa na alama zinazowatofautisha na waislamu. Vyombo vyao vya usafiri vilikuwa tofauti, mavazi yao yalikuwa tofauti. Walikuwa tofauti katika mambo mengi. Muislamu anatakiwa kujitofautisha na kafiri. Hii leo kumekuwa hakuna tofauti kati ya myahudi, mnaswara na mkomunisti. Muislamu ni lazima awe tofauti. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kujifananisha na washirikina na kusema:
“Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”
[1] Ahmad (03/50), Abu Daawuud (4031) na ´Abd bin Humayd (848). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Irwaa´-ul-Ghaliyl” (2691).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kashf-us-Sittaar, uk. 24-25
- Imechapishwa: 28/01/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kashf-us-Sittaar, uk. 24-25
Imechapishwa: 28/01/2017
https://firqatunnajia.com/muislamu-ni-lazima-ajitofautishe/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)