Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”… na utabakia uso wa Mola wako wenye utukufu na ukarimu.” (55:27)

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kutokomea isipokuwa uso Wake.” (28:88)

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?” (38:75)

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

”Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” [Siyo, bali] mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali mikono Yake imefumbuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)

وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا

”Na subiri kwa hukumu ya Mola wako – kwani hakika wewe uko kwenye macho yetu.” (52:48)

وَحَمَلْنَاهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

”Na Tukambeba kwenye ile [jahazi] iliyo [tengenezwa] kwa mbao na misumari, inatembea kwa macho Yetu.” (54:13-14)

وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِّنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي

”Na Nikakutilia mahaba kutoka Kwangu na ili ulelewe machoni Mwangu.” (20:39)

MAELEZO

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”… na utabakia uso wa Mola wako wenye utukufu na ukarimu.”

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa uso Wake.”

Hapa kuna uthibitisho wa uso wa haki. Ni uso mtukufu.

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imefumbuliwa.”

Allaah anasifika kuwa na mikono kama ambavyo vilevile Ana uso mtukufu (Jalla wa ´Alaa):

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kutokomea isipokuwa uso Wake.”

Hapa kuna uthibitisho wa uso wa haki. Ni uso mtukufu.

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imefumbuliwa.”

Allaah anasifika kuwa na mikono kama ambavyo vilevile anao uso mtukufu (Jalla wa ´Alaa).

Kadhalika anasifika kuwa na macho. Amesema (Ta´ala):

وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي

“Na ili ulelewe machoni Mwangu.”

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَ

”Inatembea kwa macho Yetu.”

Anasifika kuwa na macho, uoni na usikizi kwa njia inayolingana na Yeye (Subhaanah). Sifa zote hizi ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia inayolingana Naye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitwiyyah, uk. 37
  • Imechapishwa: 21/10/2024