Swali: Nini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… ambao hawajawahi kufanya mema kamwe.”?
Jibu: Ni lazima, hapa ni kwa isiyohusiana na upwekeshaji. Ni kama alivosema kwamba watatoka Motoni baada ya kuombea wenye kuombea ambapo Allaah atawatoa Motoni watu ambao hawajapatapo kufanya mema maishani, kwa msemo mwingine isipokuwa upwekeshaji. Allaah atawatoa Motoni kwa usiokuwa uombezi baada ya kuwa makaa na kuadhibiwa. Upokezi ndani ya ”as-Swahiyh” unasema:
”… ambao hawajawahi kufanya mema kamwe.”
Upokezi mwingine umezidisha:
”… isipokuwa tu ni kwamba wao wanasema `hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`.”
Upokezi mwingine unasema:
”… isipokuwa tu ni kwamba wao ni wapwekeshaji.”
Kwa hivyo wanazuoni wote wameafikiana juu ya kwamba mwenye kufa juu ya shirki na sio mwenye kupewa udhuru sio katika Ahl-ul-Fatrah na hasamehewi na kwamba atawekwa Motoni milele na hatotolewa humo. Mgogoro na tofauti kati yao na Mu´tazilah ni kuhusu muislamu mtenda madhambi. Ahl-us-Sunnah wanaona kuwa waislamu watenda madhambi watatolewa Motoni na kwamba hawatoadhibiwa adhabu ya milele na kwamba ni adhabu yenye ukomo. Ingawa yapo baadhi ya madhambi ambayo yanaelezea kwamba wataadhibiwa kwa kudumu, hata hivyo ni kudumu kwa muda maalum kama mfano wa kudumu kwa mzinzi na mwenye kuua mtu. Hata hivyo ni jambo lenye mwisho. Lakini kudumu kwa kafiri hakuna mwisho, bali ni kudumu milele.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24465/معنى-ما-جاء-في-الحديث-لم-يعمل-حسنة-قط
- Imechapishwa: 22/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)