Swali: Je, inafaa kwa muislamu kuhudhuria mazishi ya kafiri, kumswalia kama wanavomswalia na vivyo hivyo wakati anapozikwa?

Jibu: Hapana, haijuzu kwa muislamu kumsindikiza kafiri wala asihudhurie mazishi yake. Haijuzu kufanya hivo. Watamsimamia watu wake. Isipokuwa pale ambapo atakufa kafiri kati ya waislamu na hana yeyote, katika hali hiyo watamzika katika makaburi yasiyokuwa ya waislamu. Watamzika jangwani na mbali na mji. Katika hali hiyo ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=S4MKpPRMvvU
  • Imechapishwa: 19/02/2021