Swali: Je, inafaa kupiga kura na kuwania uchaguzi? Kwani nchi yetu haihukumu kwa Shari´ah ya Allaah.

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kuwania uchaguzi kwa kutaraji kujiunga na serikali isiyohukumu kwa Shari´ah na badala yake akahukumu kwa kanuni zilizotungwa na watu. Haijuzu kwa muislamu kumpigia kura yeyote katika serikali hii.

Isipokuwa tu ikiwa kama mtu atawapigia kura wagombea ambao ni waislamu ambao anataraji wanaweza kubadilisha hukumu na hivyo ikaongoza Shari´ah ya Kiislamu na ikaishinda ule mfumo wa serikali ulioko sasa. Hili ni kwa sharti, baada ya kuingia serikali, asifanyie kazi chochote kile kinachopingana na Shari´ah ya Kiislamu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa´imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fatwa namba. 4029
  • Imechapishwa: 19/10/2020