Swali: Je, inajuzu kwa aliye katika Ihraam kufunika uso wake?

Jibu: Sahihi ni kwamba asifunike, kwa sababu katika Hadiyth Swahiyh ya kisa cha yule aliyekanyagwa na mnyama wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wala msifunike kichwa chake wala uso wake, kwani atafufuliwa siku ya Qiyaamah hali ya kuwa ni mwenye kufanya Talbiyah.”

Swali: Je, imepokelewa kutoka kwa Salmaan kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunika uso wake?

Jibu: Imepokelewa kutoka kwa ´Uthmaan, lakini Hadiyth Swahiyh inajulisha kukataza.

Swali: Lakini kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imepokelewa kwa njia ya Hadiyth ya Salmaan?

Jibu: Sijui, bali iliyokuja ni kwa njia ya ´Uthmaan.

Swali: Kwa maana yeye ndiye alifanya hivo?

Jibu: Ndio, ni katika kitendo cha ´Uthmaan.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31075/هل-للمحرم-ان-يغطي-وجهه
  • Imechapishwa: 02/10/2025