Swali: Vipi kuhusu mtu anayevaa soksi bila kuwa na nia ya kupangusa juu yake?

Jibu: Ikiwa amevaa soksi juu ya twahara, kwa mfano wakati wa kabla ya adhuhuri, kisha ikafika wakati wa Dhuhr, basi anajuzu kupangusa juu yake hata kama hakuwa na nia ya kupangusa wakati anazivaa. Kigezo ni kuvaa soksi juu ya twahara. Akipofika wakati wa Dhuhr na akapenda kupangusa, basi anapangusa. Akipenda kuzivua atazivua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1939/حكم-من-لبس-الجورب-ولم-ينو-المسح-عليه-ثم-مسح
  • Imechapishwa: 28/12/2025