Muhammad bin Ibraahiym Aal ash-Shaykh kuhusu Saudi Arabia II

Nimesoma barua yenu – nambari 3/2758/2/1/31, tarehe 02-03-1386 – na rufaa yake kutoka kwa ubalozi wa mfalme wake mjini Cairo kuhusu swali la mahakama ya ´Aabiydiyn wakiuliza juu ya kanuni ya Saudi Arabia kwa yale yanayohusiana na matumizi ya mtoto mdogo. Napenda kuwataarifu kuwa mahakama ya Saudi Arabia – Allaah aisaidie kwa tawfiyq na uangalizi Wake – kwamba haihukumu kabisa kwa kanuni zilizotungwa na watu. Hukumu zake ni kwa Shari´ah ya Allaah (Ta´ala), Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au maafikiano ya ummah. Kwa sababu kuhukumiana kinyume na Shari´ah ya Allaah ni jambo linalopelekea katika ukafiri, dhuluma na maasi. Allaah (Ta´ala) amesema:

” وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (05:44)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (05:45)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (05:47)

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

”Na wahukumu kati yao kwa yale aliyoyateremsha Allaah na wala usifuate matamanio yao na jihadhari nao wasije kukutia kwenye mtihani ukaacha baadhi ya yale aliyokuteremshia Allaah. Na wakikengeuka, basi tambua ya kwamba hakika Allaah anataka kuwaadhibu kwa baadhi ya madhambi yao; na hakika wengi katika watu ni mafasiki. Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.” (5:49-50)

Muftiy wa Saudi Arabia

1386-11-21

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/341)
  • Imechapishwa: 24/03/2024