Swali: Vipi tutaoanisha baina ya kutohama mtu na maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
”Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya.”[1]
Jibu: Hii ni kwa yule anayewafanya marafiki na kushirikiana nao katika mambo yao. Lakini wewe, haufanyi urafiki nao. Bali unawasiliana nao kwa ajili ya ulinganizi, si kwa ajili ya urafiki. Unawasiliana nao kwa ajili ya kuwaita katika kheri, kuwaongoza na kuwapa nasaha, lakini si kuandamana nao katika maovu yao. Wana wa israaiyl walikuwa wakiandamana nao katika maovu yao na wakaacha kuwakataza. Ama wewe, unapotembelea unamkataza, unamuamrisha mema na unamkataza maovu, mara mbili au tatu. Huenda akaongoka, lakini bila kumfanya rafiki wako wa karibu wa kula na kunywa pamoja naye.
Swali: Kuna muda maalum wa kumhama mtu?
Jibu: Inategemea jitihada ya anayehama. Hakuna muda maalum.
Swali: Je, amsalimie?
Jibu: Asimsalimii wala asipeane naye mkono, hata kama miaka ikipita muda wa kuwa bado yuko juu ya Bid´ah yake au maovu yake ya dhahiri.
Swali: Je, kuna muda maalum wa kutoa nasaha?
Jibu: Kila ukikutana naye, mpe nasaha. Kila itakapotokea fursa, mpe nasaha. Akikataa na kuendelea kushikamana na upotovu, ndipo unamhama.
Swali: Kumhama mtu katika mambo ya dunia ni kwa muda wa siku tatu?
Jibu: Ndiyo, kumhama katika mazungumzo ni kwa siku tatu. Allaah akimwongoza, hilo ni kwa haki yake binafsi, si kwa haki ya Allaah, bali ni haki baina ya watu.
Swali: Je, ni sahihi wale wanaosema kuwa kuhama katika zama hizi hakufai?
Jibu: Hapana, ni kosa. Kuhama bado kuna faida. Ikiwa watu wa kheri, wanazuoni na wenye mamlaka watamhama, hakika itakuwa na athari. Ikiwa haitakuwa na athari, basi umeshatimiza wajibu wako na imetakasika dhimma yako.
[1] 05:79
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31627/ما-مدة-الهجر-الشرعي-وكيفيته
- Imechapishwa: 12/11/2025
Swali: Vipi tutaoanisha baina ya kutohama mtu na maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
”Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya.”[1]
Jibu: Hii ni kwa yule anayewafanya marafiki na kushirikiana nao katika mambo yao. Lakini wewe, haufanyi urafiki nao. Bali unawasiliana nao kwa ajili ya ulinganizi, si kwa ajili ya urafiki. Unawasiliana nao kwa ajili ya kuwaita katika kheri, kuwaongoza na kuwapa nasaha, lakini si kuandamana nao katika maovu yao. Wana wa israaiyl walikuwa wakiandamana nao katika maovu yao na wakaacha kuwakataza. Ama wewe, unapotembelea unamkataza, unamuamrisha mema na unamkataza maovu, mara mbili au tatu. Huenda akaongoka, lakini bila kumfanya rafiki wako wa karibu wa kula na kunywa pamoja naye.
Swali: Kuna muda maalum wa kumhama mtu?
Jibu: Inategemea jitihada ya anayehama. Hakuna muda maalum.
Swali: Je, amsalimie?
Jibu: Asimsalimii wala asipeane naye mkono, hata kama miaka ikipita muda wa kuwa bado yuko juu ya Bid´ah yake au maovu yake ya dhahiri.
Swali: Je, kuna muda maalum wa kutoa nasaha?
Jibu: Kila ukikutana naye, mpe nasaha. Kila itakapotokea fursa, mpe nasaha. Akikataa na kuendelea kushikamana na upotovu, ndipo unamhama.
Swali: Kumhama mtu katika mambo ya dunia ni kwa muda wa siku tatu?
Jibu: Ndiyo, kumhama katika mazungumzo ni kwa siku tatu. Allaah akimwongoza, hilo ni kwa haki yake binafsi, si kwa haki ya Allaah, bali ni haki baina ya watu.
Swali: Je, ni sahihi wale wanaosema kuwa kuhama katika zama hizi hakufai?
Jibu: Hapana, ni kosa. Kuhama bado kuna faida. Ikiwa watu wa kheri, wanazuoni na wenye mamlaka watamhama, hakika itakuwa na athari. Ikiwa haitakuwa na athari, basi umeshatimiza wajibu wako na imetakasika dhimma yako.
[1] 05:79
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31627/ما-مدة-الهجر-الشرعي-وكيفيته
Imechapishwa: 12/11/2025
https://firqatunnajia.com/muda-wa-kumhama-mzushi-au-mtenda-maasi/