Muadhini atoke nje ya msikiti?

Swali: Imepokelewa katika baadhi ya vitabu vya Sunnah kwamba muadhini wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoa adhaana nje ya msikiti, katika mlango wake. Je, hili ni jambo la Sunnah ya lazima au ya kupendeza tu?

Jibu: Hapana, Hii ni Hadiyth dhaifu iliyopokelewa na Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi dhaifu, kwa sababu ni kupitia njia ya Ibn Ishaaq ambaye amepokea kwa njia isiyo wazi na hali ya kuwa ni mwenye kufanya hadaa. Hivyo Hadiyth yake inapokuwa kwa mfumo wa undanganyifu inakuwa dhaifu na haithibitiki. Sunnah katika adhaana ni kuwa muadhini awe katika sehemu ya juu, kama vile Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh) alivyokuwa akitoa adhaana juu ya paa, ili sauti iwe na upeo mkubwa zaidi. Ikiwa kuna mnara, kama ilivyo desturi ya watu kujenga minara, basi hilo pia linaongeza upeo wa sauti. Katika zama hizi ambapo kuna vipaza sauti, watu wamekuwa wakitosheka navyo kwa sababu inakuza sauti na kuifikisha mbali. Kwa sababu hiyo baadhi ya watu wameacha kutegemea minara kwa kuwa kipaza sauti kinatosheleza mahitaji ya kusikika kwa adhaana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1123/هل-صح-انه-كان-يوذن-خارج-المسجد
  • Imechapishwa: 30/01/2026