Swali: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha Mitume kabla au baada ya safari ya kwenda juu mbinguni?
Jibu: Kwa mujibu wa “as-Swahiyh” ya Muslim aliwaswalisha, lakini hakukutajwa chochote kama alifanya hivo kabla au baada ya safari ya kwenda juu mbinguni. Imaam Muslim (Rahimahu Allaah) amesema: Zuhayr bin Harb ametuhadithia: Hujayn bin al-Muthannaa ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Fadhwl, kutoka kwa Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nilipokuwa karibu na jumba la mawe (الحِجر), Quraysh waliniuliza kuhusu safari yangu ya Usiku. Wakaniuliza mambo kuhusu Yerusalemu ambayo nilikuwa sikuyadhibiti. Ndipo Allaah akaninyanyulia mji ili niweze kuuona; hawakuniuliza chochote isipokuwa niliwajibu. Nilikuwa miongoni mwa kundi la Manabii. Nikamuona Muusa amesimama akiswali. Nikamuona mtu mwenye nywele zilizosokotwa utasema ni katika watu wa Shaanu-ah – alikuwa ni ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) amesimama akiswali. Mtu ambaye anafanana naye zaidi alikuwa ni ´Urwah bin Mas´uud ath-Thaqafiy. Nikamuona Ibraahiym (´alayhis-Salaam) amesimama akiswali. Mtu ambaye anafanana naye zaidi ni mwenzenu (bi maana yeye mwenyewe). Ukafika wakati wa swalah na nikawaswalisha. Nilipomaliza kuswali akasema msemaji: “Ee Muhammad! Huyu ni Maalik, mlinzi wa Moto. Msalimie.” Nikamgeukia na yeye ndiye akaanza kunisalimia.”[1]
[1] Muslim (172).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 316-317
- Imechapishwa: 20/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket