Swali: Tunawezaje kuoanisha baina ya Hadiyth ya ´Aaishah:

”Hakika mkono wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haujapatapo kugusa mkono wa mwanamke kamwe.”

na yale yaliyokuja katika ”as-Swahiyh” ya kwamba:

”Kijakazi alimshika mkono Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka akamtimizia haja yake.”?

Jibu: Kijakazi hana hukumu sawa na mwanamke huru. Kijakazi alikuwa akiuzwa na kununuliwa. Kwa ajili hiyo kijakazi hajisitiri hata mbele ya wanaume wa kando naye. Aida inawezekana kwamba huyo alikuwa kijakazi mdogo, jambo ambalo ndilo lililo karibu zaidi na usahihi. Kwa msemo mwingine alikuwa bado hajafikia umri wa kubaleghe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 26/09/2026