Swali 3716: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahi kunyoa kichwa chake na ndevu zake katika maisha yake?

Jibu: Imethibiti ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinyolewa kichwa chake wakati wa kujitwaharisha kutoka katika Hajj ya Kuaga. Lakini haijathibiti kwamba aliwahi kunyoa ndevu zake, si wakati wa kujitwaharisha kutoka katika ´ibaadah ya Hajj wala wakati mwingine wowote. Bali imethibiti kwamba aliziacha ndevu zake zikue na hakukata chochote kabisa.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/153)
  • Imechapishwa: 23/10/2026