Swali 4666: Je, inajuzu kwangu kunyoa mashavu mawili na kuacha ndevu? Je, inajuzu kwangu kunyoa nikiwa nimefunga na ikiwa damu itatoka, ni mamoja ikiwa ni kunyoa kichwa, nywele za sehemu za siri au nyinginezo?

Jibu: Haijuzu kunyoa ndevu za mashavuni, kwa sababu ni miongoni mwa ndevu. Inajuzu kwa mwanaume kunyoa kichwa chake, nywele za sehemu za siri na mfano wake katika Ramadhaan na miezi mingine, hata ikiwa damu itatoka. Bali kunyoa nywele za sehemu za siri ni miongoni mwa Sunnah za kimaumbile.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/158)
  • Imechapishwa: 23/10/2026