Mtume (´alayhis-Salaam) hakuweka kikomo sha swalah ya usiku

Swali: Ikiwa Imamu anaswali Tarawiyh Rakaa ishirini, je, nikiswali pamoja naye Rakaa kumi kisha nikatoka nakuwa nimefuata Sunnah na nimekosa fadhila za kusimama [usiku mzima] na Imamu?

Jibu: Ikiwa anaswali Rakaa ishirini na tatu kamilisha naye.

“Mwenye kuswali nyuma ya Imamu mpaka akamaliza, Allaah Humwandikia kama amesimama Qiyaam-ul-Layl nzima.”

Swali pamoja naye mpaka akamilishe. Jambo hili ni sahali kuhusu kisimamo cha Ramadhaan. Anayetaka anaweza kuswali Rakaa 11, 13, 23 au zaidi. Jambo hili ni sahali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Swalah ya usiku ni (Rakaa) mbili mbili. Akikhofia (kuingia kwa) Subh aswali Rakaa moja awitiri kwayo.”

Hakuweka mpaka. Hakusema ni Rakaa 10, 20 na kadhalika. Hakuweka mpaka katika Swalah ya usiku, bali amesema:

“Swalah ya usiku ni (Rakaa) mbili mbili.”

Hata kama ataswali Rakaa mia, jambo hili ni sahali. Lakini bora zaidi ni Rakaa 13 au 11. Hili ndio bora zaidi kama alivyokuwa akifanya yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mara nyingi alikuwa akiswali hizi (Rakaa 11).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12827
  • Imechapishwa: 05/05/2015